Mkurugenzi wa wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar – TAMWA-ZNZ, Dkt. Mzuri Issa, amewashauri  wanawake na Vijana kujiamini na kuondosha woga wakati wa kugombea nafasi za Uongozi, ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Dkt. Mzuri ameyasema hayo akifungua mafunzo ya siku mbili ya uongozi kwa vijana wa kike, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuungana kuleta ushawishi katika maendeleo ya agenda mbalimbali za kitaifa na kudai kuwa Dunia imetambua umuhimu kutokana na maendelo yaliyoletwa na viongozi wanawake.

Amesema, “Mwanamke ni Kiongozi bora, na nyinyi vijana ndio tunawategemea muwe na maono ya mbali katika kuleta uongozi ulio imara na kuibeba  nafasi ya mwanamke katika uongozi, mwanamke anaweza kuwa mama, mke, mfanyakazi na kiongozi na wakati huohuo na akaweza kutekeleza  majukumu yote hayo na akafanya vizuri katika kila sekta.”

Akitoa mafunzo hayo kwa vijana wa kike 15, Mkufunzi wa masuala ya Uongozi, Imelda Lulu Urrio amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kujitambua na kutambua nafasi zao ili kufikia ndoto zao katika harakati za Uongozi.

Amesema, “nafasi ya wanawake kwa sasa inazidi kuongezeka kwa sababu kuna ukuwaji wa Elimu kwa jamii na hata watoto wa kike wenyewe wameanza kujitambua na kujielewa, tumeona baadhi ya jamii inavyowajenga watoto wa kike kujitambua na kupelekea ongezeko kubwa la viongozi wanawake.”

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za Uongozi – SWIL, unaotekelezwa na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway Wanawake wameachwa nyuma katika ngazi za maamuzi, hivyo Wanawake watumie fursa na haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa ili kufikia  dhamira ya 50/50 katika masuala ya uongozi.

Young Africans kuweka rekodi Afrika
Bima ya Afya kupunguza gharama za matibabu - Dkt. Mollel