Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) imepata tuzo ya dhahabu miongoni mwa washindi 51 kutoka nchi 39 duniani wa tuzo ya huduma za viwango zinazotolewa na taasisi ya European Society For Quality research (ESQR).

Taarifa toka TANAPA inaeleza kuwa tuzo hizo za huduma bora hutolewa kila mwaka na shirika la ESQR kwa kutambua taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na watu binafsi wanatoa huduma za viwango vya juu.

Washindi wa tuzo hizi uchaguliwa kwa kuzingatia matokeo ya kura zilizopigwa na taasisi zilizoshinda tuzo hii awali , maoni ya wateja na utafiti wa masoko.

mchakato wa upatikanaji wa washindi wa tuzo hii umejumuisha utafiti wa taarifa mbalimbali za umma , machapisho ,maoni chanya ya wateja ,miradi ya kijamii na vyuo vikuu pamoja na maonesho.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji Jestas Nyamanga atapokea tuzo hiyo mapema wiki ijayo kwa niaba ya shirika la hifadhi taifa Tanzania jijini Brussels, Ubeligi.

EUROPA LEAGUE: Mourinho ashtukia jambo Spurs
Marekani kuvaa barakoa kwa siku 100