Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.

Wakati Tapasisi mbalimbli zikiendelea kutoa misaada Kwa waathiirika wa Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya maji na mawe katika mji wa katesh Mkoani Manyara na zoezi la ukoaji likiwa bado linaendelea, Shirika la Hifadhi la Taifa – TANAPA, limetoa Askari wake 19 kusaidia zoezi hilo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Kamishna wa TANAPA, Mussa Nassor wakati alipofika Hanang’ kujionea hali halisi ya tukio hilo na kutoa pole kwa Wananchi pamoja na Serikali kwa ujumla.

Amesema, mbali na kutoa Askari hao, pia TANAPA pamoja inaahaidi kutoa kiasi cha Shilingi 10 Million zikilenga kusaidia katika zoezi hilo la ukoaji pamoja na waathiirika.

Gamondi: Tutapambana ili tushinde hapa Ghana
Pauni Milion 60 kumng'oa Douglas Luiz