Timu ya taifa ya riadha ya Tanzania itayokwenda kwenye michuano ya Olimipiki imepata udhamini wa vifaa vya michezo pamoja na fedha za kiasi cha shilingi milioni tano.

Udhamini huo umetolewa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo na kukabidhiwa kwa wachezaji hao.

Ufadhili huo unalengo kuisadia timu ya taifa na kuwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Olimpiki na pia kusaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Baada ya kupata ufadhili huo, Rais wa shirikisho la riadha RT Antony Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kulipia kadi za bima ya afya ya wachezaji hao na familia zao kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji hao, Alfonce Felix amesema ufadhili huo utawaongezea chachu ya ushindi na kuitangaza nchi.

Timu hiyo ya riadha yenye wachezaji wanne inaendelea na maandalizi ya mwisho chini ya kocha wake Francis John katika kambi ya West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.

Mapacha wa P Square watangaza rasmi kumaliza ‘bifu’ kati yao
Azam FC Yahamishia Kambi Visiwani Zanzibar