Shirika la Umeme nchini (TANESCO), linatarajia kufanya maboresho katika mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa kabla (LUKU), katika kituo chake cha kujikinga na majanga ambayo yataathiri upatikanaji wa huduma ya malipo.

Kwa mujibu wa msemaji wa TANESCO Martine Mwambene, amesema maboresho hayo yatakayofanyika usiku wa Juni 9, 2022 yatasababisha wateja kukosa huduma kwa muda wa saa mbili.

“Maboresho haya yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuwahudumia wateja ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yoyote katika kituo kikuu cha mifumo ya luku ya shirika,” amesema.

Mwambene ameongeza kuwa sema ya wateja 5,000 wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao ni sawa na asilimia 90, wameunganishiwa umeme kupitia huduma ya Nikonect iliyoanzishwa na shirika hilo hivi karibuni.

Hata hivyo, amewataka wateja kujiunga na huduma hiyo inayopatikana kupitia simu za viganjani hasa pale wanapohitaji kuunganishiwa umeme, ili kuondoa usumbufu.

ADF yahusishwa mauaji watu 20 DRC
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 07, 2022