Shirika la umeme Tanzania (Tanesco)limesema kuwa litachukua hatua kali dhidi ya wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakilihujumu ikiwamo kuwafukuza kazi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani katika uzinduzi wa mradi wa awamu ya tatu wa usambazaji umeme vijijini REA uliofanyika katika kijiji cha Kirya Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
“Watumishi wote wa umma waliozoea kucheza dili chafu na vishoka na kuhujumu miradi ya umeme wakati wa kuwaunganishia wananchi umeme dawa yao imeiva, tutawafukuza kazi wale wote watakaobainika kufanya uhujumu,”amesema Kalemani
-
Msukuma amkumbuka Nape sakata la Bombardier
-
NEC yateuwa Madiwani 12 wanawake wa viti maalum
-
Video: Makonda kusaidia watu 1000 miguu ya bandia
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo amesema kuwa awamu ya tatu ya mradi huo katika mkoa wa Kilimanjaro utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 24.