Shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) limewataka wafanyabiashara wadogo wadogo waliopo maeneo ya vituo vya Daladala/Mabasi kufuata utaratibu uliowekwa na shirika hilo kuunganishiwa huduma umeme.

TANESCO imetoa muda wa miezi mitatu kwa wafanyabiashara  hao kuhakikisha wanafuata utaratibu, badala ya kujiunganishia kiholela ili kuepuka madhara yatokanayo na umeme.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa wa miondombinu eneo la Mbezi Louis jijini Dar es Salaam, Meneja wa wateja wakubwa wa shirika hilo Fredrick Njavike, amesema kuwa  kujiunganishia umeme kunahatarisha maisha yao.

“Nitoe rai kwa wananchi wote kufuata taratibu wa kuunganishiwa umeme na wawe wazalendo kwa nchi yao, kwa kuacha kuhujumu miundombinu ya shirika. Kwani licha ya shirika kupata hasara bado wafanyabiashara wanahatarisha maisha yao,”.

TANESCO wamekuwa na utaratibu wa kutoa  elimu kwa wateja wake ili kupunguza ajali na matatizo ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

PSG wapambania haki, kushirikiana na LFP
Ivory Coast: Mahakama yamuidhinisha Ouattara kugombea urais