Mkoani Mtwara, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kukatika kwa umeme katika mkoa huo kunatokana na kasi kubwa ya wananchi kuunganisha umeme, hivyo uzalishaji wa umeme unaofanywa na shirika hilo kuwa mdogo.
Menenja wa TANESCO mkoa wa Mtwara Fadhili Chilombe amesema ofisi yake inalitambua tatizo hilo ambalo linatokana na uzalishaji wa umeme kuzidiwa na wateja.
Waganga wa kienyeji kusajili vitendea kazi vyao
Aidha amesema kuwa tayari serikali imenunua mitambo mipya ambayo itafungwa ili kuondoa Tatizo hilo katika mkoa wa Mtwara.
Hatahivyo wakazi wa mkoa huo wameomba shirika hilo kurekebisha tatizo la umeme kuwaka na kuzima na mara kwa mara hivyo kupelekea hata thamani zao za ndani kuugua.