Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme. Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi. TAHADHARI Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo. Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.

TANESCO inawaomba ushirikiano na kuwa waangalifu wakati wa zoezi hili. Kwa mawasiliano Tovuti: www.tanesco.co.tzMitandao ya Kijamii www.facebook/tanescoyetu twitter.com/tanescoyetu

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka Kwa taarifa za dharura kituo cha Miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO, TANESCO – MAKAO MAKUU.

Novemba 18, 2017

 

Watuhumiwa dawa za kulevya kuhukumiwa jela maisha
RC Geita aagiza ukaguzi wa mapato ufanyike