Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, limeutaarifu Umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika Gridi ya Taifa hii leo Desemba 8, 2023 majira ya saa 04:14 asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Makao Makuu Dodoma, imeeleza kuwa hitilafu hiyo ilipekea Mikoa inayopata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.
Aidha, hitilafu imetokana na kusombwa na maji nguzo kubwa za kusafirisha Umeme kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III eneo la Mto Gide, Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam.
Uharibifu huo umepelekea kutoka kwa Gridi ya Taifa na kwamba Umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo.
Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa jitihada nyingine zinazofanywa na Shirika ni kuhakikisha miundombinu iliyoharibika inajengwa ndani ya muda mfupi, kuruhusu kusafirisha umeme unaokosekana katika Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III.