Shirika la umeme Tanzania, (Tanesco) limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa linawataka wateja wake kununua umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu, hivyo kupelekea kuathiri mfumo wake wa LUKU.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya shirika hilo imesema kuwa taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ni ya kizushi na haina ukweli wowote.
Shirika hilo limewataka wateja wake kupuuza taarifa hiyo, kwani huduma zote za umeme ikiwemo manunuzi ya LUKU zinaendelea kutolewa kama kawaida.
-
Taasisi ya TYCEN yaanzisha Club Shule za Sekondari
-
Serikali kutoa Leseni kwa Hospitali na vituo vya Afya
-
JPM amuandikia barua Rais wa China
Hata hivyo, Shirika hilo limewataka wananchi kutozisogelea wala kushika nyaya zilizokatika au kuanguka sehemu mbalimbali.