Shirika la umeme Tanzania, (Tanesco) limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa linawataka wateja wake kununua umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu, hivyo kupelekea kuathiri mfumo wake wa LUKU.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya shirika hilo imesema kuwa taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ni ya kizushi na haina ukweli wowote.

Shirika hilo limewataka wateja wake kupuuza taarifa hiyo, kwani huduma zote za umeme ikiwemo manunuzi ya LUKU zinaendelea kutolewa kama kawaida.

Hata hivyo, Shirika hilo limewataka wananchi kutozisogelea wala kushika nyaya zilizokatika au kuanguka sehemu mbalimbali.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 28, 2017
Video: Mpina atangaza vita dhidi ya uvuvi haramu