Shirika la Umeme Tanzania, Tanesco linautaarifu umma na wateja wake wote kuwa wametoa siku nne kwa wadaiwa wake sugu kuhakikisha wanakamilisha madeni yote ambayo wanadaiwa.

Ambapo wametangaza siku nne hizo ni kuanzia siku ya kesho, 12 Januari 2018 hadi siku ya tarehe 15 januari 2018.

Aidha wamesema kuwa baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Hivyi Ofisi za Tanesco zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

kwa mawasiliano zaidi wamesisitiza kupiga namba ya kituo cha miito ya simu Mako Makuu ambayo ni +255 222 194 400 na +255 768 985 100

 

Video: Diamond Platnumz aonyesha jengo lake jipya la WCB
Ole Sendeka amcharukia Mange Kimambi