Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewaomba radhi wateja wake wote wa mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifa kwa kukosa huduma ya umeme siku ya jana Alhamisi, Septemba 27, 2018, majira ya Saa 7:42 Mchana.
Aidha, shirika hilo limesema kuwa sababu kubwa iliyosababisha kukosekana kwa huduma hiyo ni hitilafu katika transfoma ya 220/33 kV ya kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Kidatu (Kidatu switch yard).
“Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na jitihada za kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida, hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza,” imesema taarifa hiyo
-
CDF athibitisha kivuko cha MV Nyerere kunyanyuka
-
Breaking News: Rais Magufuli akizindua Flyover muda huu
-
JPM ataja sababu ya kuita Mfugale flyover