Gazeti la Daily Express linaripoti kuwa Chelsea wapo kwenye mpango wa kumyakua kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini.

Pellegrini mwenye uraia wa Chile, ambaye anataraji kufikisha miaka 63 baadaye mwaka huu, amesema kuwa ataondoka kunako klabu ya City mwishoni mwa msimu,  huku nafasi yake ikitarajiwa kujazwa na kocha wa sasa wa Bayern Munich Pep Guardiola.

Kwa mujibu wa Pellegrini, bado yuko tayari kusikiliza ofa kutoka sehemu mbalimbali kabla ya kuamua kustaafu rasmi kufundisha soka, huku Chelsea wakionekana kama klabu namba moja kwenye mbio za kumwania kocha huyo.

Wasaka Nyoka Tanzania Bara Kuumana Tena Kesho
Jamal Malinzi Ampongeza Jakaya Mrisho Kikwete