Mamlaka ya magereza nchini Ecuador, imesema watu wasiopungua 10 wamekufa katika machafuko yaliyotokea katika gereza la El Inca lililopo kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Quito.

Kamanda wa Polisi wa Eneo hilo, Victor Herrera amesema ulinzi mkali umewekwa karibu na gereza hilo wakati maafisa wa uchunguzi wakiondoa miili ya waliouawa, na kudai kuwa sababu ya vifo hivyo inahisiwa kuwa ni uwezekano wa kunyongwa.

Ulinzi katika Gereza la El Inca baada ya tukio. Picha ya Dolores Ochoa/ AP.

Vurugu katika Gereza hilo, zilizuka baada ya taarifa ya Serikali kubaini kuwa ingewahamisha wafungwa wawili, ambao wanashukiwa kuhusika na ghasia za hapo awali kwenye gereza hilo lenye ulinzi mkali.

Tangu mwaka jana (2021), vurugu katika jela nchini Ecuador zimesababisha vifo vya wafungwa wapatao 400 kitu ambacho kimesababisha mashirika ya kutetea haki za Binadamu kuendelea kupaza sauti kwa mamlaka za nchi hiyo kuchukua hatua stahiki.

Urusi yaharibu nusu ya mifumo ya umeme Ukraine
Kagame kumsadia Kenyatta kusitisha mapigano