Wasiwasi wa matumizi ya jina la Kilimanjaro Stars ambalo hutumiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara kinaposhiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup, umetanda kwa kiasi kikubwa kutokana na udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti.
Wasiwasi huo umeibuliwa na aliyekua mwanasheria wa shirikisho la soka nchini TFF wakati wa utawala wa Jamal Malinzi Emmanuel Muga, ambapo amesema kuna hatari kubwa ya kuvunja mkataba uliopo kati ya shirikisho hilo na kampini ya bia ya Serengeti (SBL) ambayo ndio mdhamini mkuu wa timu ya taifa.
Muga amesema matumizi ya jina la Kilimanjaro Stars, yatakua yanakwenda kinyume na mkataba uliosainiwa na uongozi wa TFF uliopita, kwani alishiriki katika kila hatua ya makubaliano yaliyofikiwa.
-
Amr Fahmy kuendesha shughuli za utendaji CAF
-
Tanzania bara yapangwa na Zanzibar CECAFA Challenge Cup 2017
Hata hivyo inafahamika kuwa, Taifa Stars ni timu ya taifa ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, na Kilimanjaro Stars ni timu ya Tanzania bara pekee.
Timu ya Kilimanjaro Stars kitashiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup itakayoanza Desemba tatu hadi kumi na saba, na imepangwa katika kundi A, sambamba na wenyeji Kenya, Zanzibar, Libya pamoja na Rwanda.
Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.