Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano – JPC, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta za kipaumbele hususan bishara na uwekezaji, afya, uchukuzi, elimu, utamaduni, uchumi wa buluu na maeneo mengine.

“Tanzania itaendelea kushirikiana Comoro ili kuendeleza ushirikiano uliodumu kwa kipindi kirefu kwa maslahi ya pande zote mbili hususan katika sekta za biashara na uwekezaji,” amesema Dkt. Tax

Kwa upande wake Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema kwamba Comoro inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania ambapo uhusiano huo umekuwa imara na umedumu kwa muda mrefu.

Wanawake CHADEMA wafundwa fursa kiuchumi, matumizi ya Fedha
Ufungaji wa Makanisa ni njama kuzuia Injili - Mchungaji Odero