Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkaribisha mgeni wake
Rais wa Hungary, Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam hii leo Julai 18, 2023 katika ziara inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizi mbili.

Mara bada ya kuwasili Ikulu, mgeni huyo akiongozwa na mwenyeji wake Rais Samia, walishuhudia vikundi mbalimbali vya ngoma, na baadaye kuzungumza na vyombo vya Habari huku ikielezwa kuwa Watanzania wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa masomo katika Vyuo Vikuu vya Hungary.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake
Rais wa Hungary, Katalin.

Watanzania hao hunufaika kwenye fani za shahada ya kwanza, shahada za uzamili na shahada za uzamivu ambapo kozi ambazo Hungary imekuwa ikifadhili kwa Watanzania ni zile za kimkakati ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

Kwa miaka mingi msaada wa kiufundi wa Hungary kwa Tanzania, umekuwa ukilenga sekta ya Elimu hususan ufadhili wa masomo kwa Watanzania kwenda Hungary na matukio ya kisiasa na kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 90 yalisababisha kupungua shughuli za Hungary barani Afrika, ikiwemo Tanzania.

Kitayosce yaitaka saini ya Kocha wa Simba SC
FIFA kuchelewesha dilila De Gea Uarabuni