Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Dkt. Qu Dongyu amesema Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza sekta ya kilimo na uchumi wa buluu, hivyo Shirika lao lipo tayari kutoa ushirikiano katika kutoa msaada wa kitaalam pamoja na kukuza mifumo ya uzalishaji wa chakula.

Dkt. Qu Dongyu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi  Oktoba 20, 2023, huku Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamata Shaame Hamisi akisema Serikali inafanya maboresho katika sekta ya kilimo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji inayolenga kuimarisha upatikanaji wa chakula.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alisema Serikali imeendelea kuwashawishi vijana kushiriki katika shughuli za kilimo kwani mbali na kuongeza uzalishaji wa chakula, pia kilimo ni miongoni mwa sekta zinazotoa ajira nyingi, hivyo watakuwa wamejihakikishia ajira.

Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Italia Mhe. Sergio Mattarella na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Ireland Mhe. Michael Higgine, Rais wa Iraq Mhe. Abdul Latif Rashid, Mfalme wa Lesotho, Viongozi wa Ujumbe kutoka Nchi Wanachama, Viongozi Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (FAO, IFAD & WFP).

Rais Biden chupuchupu Jordan
Kero ya Maji: DC Malisa aipa maagizo RUWASA