Taarifa kutoka Ikulu imesema Mataifa ya Tanzania na India, sasa yamebadili uhusiano wao kutoka ule wa kawaida Kidiplomasia na kuwa wa Kimkakati.
Hatua hiyo, imefikiwa kufuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Samia Suluhu Hassan inayoendelea nchini India, ambapo leo imetangazwa rasmi kwenye mkutano wake na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.
Tofauti kati ya ushirikiano wa kidiplomasia na ule wa kimkakati, hasa unaohusu India, ni kuwa nchi zote zinakuwa zimechagua maeneo mahususi ya kushirikiana yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Mazungumzo ya kufikia kufanya biashara kwa kutumia Shilingi na Rupia na kuongeza ushirikiano kwenye huduma za afya, ulinzi na kubadilishana taarifa sasa yatawezekana kwa sababu ya TZ na India kufikia hatua hii.
Huu ni ushindi mkubwa kwa Diplomasia ya Tanzania chini ya Rais Samia, ikizingatiwa kuwa haya ni makubaliano dhidi ya nchi tajiri na yenye ushawishi mkubwa duniani.