Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia makabidhiano ya hati sita kati ya 14 zilizosainiwa baina ya India na Tanzania, zikihusisha taasisi za Serikali na sekta binafsi.

Hati hizo zinajumuisha;

  1. Hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Elektroniki na Teknolojia ya Habari ya India na Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ushirikiano katika nyanja ya kupeana suluhu zenye mafanikio za kidijitali zinazotekelezwa kwa ujuzi wa idadi ya watu kwa ajili ya mabadiliko ya kidijitali.
  2. Mabadilishano ya Hati ya makubaliano ya kiufundi kati ya Jeshi la Wanamaji la India na Shirika la Wakala wa Meli wa Tanzania kuhusu kupeana taarifa za meli za kibiashara.
  3. Hati ya makubaliano ya mpango wa kubadilishana utamaduni kati ya India na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka ya 2023 – 2026.
  4. Hati ya makubaliano kati ya Baraza la Michezo la Taifa la Tanzania na Mamlaka ya Michezo ya India kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Michezo.
  5. Hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Bandari ya Jawaharlal Nehru chini ya Wizara ya Usafirishaji wa Bandari na Njia za Majini ya India na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa ajili ya kuanzisha Kongani ya Biashara nchini Tanzania.
  6. Hati ya makubaliano kati ya Coaching Shipyard Limited na Marine Services Cooperation Limited kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa Majini.

Mbali na mikataba hiyo, Tanzania na India wamesaini pia mkataba mmoja inayofanya jumla ya nyaraka zilizosainiwa kufikia 15.

Vijana changamkieni fursa Ujenzi Vituo vya Mafuta Vijijini - Kapinga
DCEA yateketeza ekari 807, kukamata shehena ya Bangi