Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema Tanzania iko vizuri na inakopesheka na kwamba hakuna Mtanzania atakaye gongewa mlango ili kutakiwa kulilipa deni la Taifa ambalo linaongezeka.

Mwigulu ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha Habari cha jijini Dar es Salaam, hii leo Desemba 14, 2022 na kuongeza kuwa deni la Taifa linaongezeka kwani hata kukamilika kwa kipande cha reli ya kisasa Morogoro – Dar es Salaam kunahitaji malipo.

Amesema, “Deni la Serikali kwa uwiano wa pato la Taifa ni 32.5% ukomo wa juu uliowekwa ambao haupaswi kuvuka, deni la nje kwa pato la Taifa tupo asilimia 18.1 na ukomo wa juu ni asilimia 40, hatujavuka hata nusu yake, sisi tunakopesheka na tupo vizuri sana.”

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, akionea jambo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha Waziri Mwigulu pia amesema, “Hakuna atakayeambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa, ni kama mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakayekwenda kuchukua madaftari ya Mwanafunzi.”

Kuongezeka kwa deni la taifa, la kiasi cha Shilingi 21 trilioni ndani ya miezi 6 kumezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ambapo taarifa ya uchumi iliyotolewa hivi karibuni na BoT inaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi Oktoba 2022 deni la taifa lilikuwa limefikia Shilingi 90.35 trilioni.

Mustapha Hadji: Morocco itashangaza Dunia
Zoran Maki akalia kuti kavu Misri