Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania na Kenya vimepanga kushirikiana katika kudhibiti vitendo vya uhalifu wa mipaka ili kuzuia vitendo vya uharamia, madawa ya kulevya, ujangili na biashara ya kusafirisha watu (Human trafficking).
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati alipokutana na kuzungumza na Rais wa Kenya, William Ruto Ikulu Jijini Dar Es Salaam hii leo Oktoba 10, 2022.
Rais Samia amesema, vitendo vya uhalifu vinavyovuka mkapa vimekuwa vikileta sura mbaya katika rekodi ya Dunia na kuwataka viongozi wa Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa ukaribu kuzuia vitendo hivyo na kuimarisha usalama ulioasisiwa na Viongozi waliotangulia.
Amesema, ”Tumezungumza pia kushirikiana kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyovuka mpaka na hapa tumekubaliana kuwataka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kushirikia kwa ukaribu na kuzungumza kuangalia makosa yanayovuka mpaka, madawa ya kulevya uharamia, kwenda kuuwa wanayama ujangili lakini pia maswala ya kusafirisha watu human trafic.”
Aidha, ameongeza kuwa ”Tumekuwa tunapata sifa mbaya ya human trafic wakati wanaosafirishwa sio watanzania sisi tunakamata tu lakini wakifika kwetu rekodi za dunia zinaiona Tanzania au Kenya inabidi tuangalie vizuri.”
”Jambo jingine ni kushirikiana katika maswala ya kikanda na kimataifa na hapa tumekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri na madhubuti kwenye umoja wa Afrika kule UN lakini hasa ndani ya Afrika Mashariki kwamba Kenya, Tanzania na Uganga ndiyo viongozi wakubwa wa Jumuiya hii hivyo hatuna budi kushiriana ili wanaoungana nasi wakute kuna ushirikiano madhubuti uliojengwa nasi” amesema Rais Samia.