Tanzania imeanza kukabidhi uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Afrika SADC kwa nchi ya Msumbiji kwa njia ya mtandao kupitia mabalozi wa nchi hizo mbili kufuatia changamoto ya ugojnwa wa COVID-19.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Ibuge.

Amesema kuwa balozi wa Msumbiji nchini, Monica Musa atakabidhiwa uenyekiti wa SADC kwa niaba ya nchi yake, hivyo hivyo pia balozi wa Tanzania nchini Msumbiji atakabidhi uenyekiti kwa serikali ya Msumbiji kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Aidha Brigedia Jenerali Ibuge amesema kwa nafasi yake ya katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki atakabidhi uenyekiti wa makatibu wakuu wa nchi za SADC kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Msumbiji kupitia balozi wa Tanzania nchini humo.

Ameongeza kuwa Agosti 13 2020, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba kabudi naye atakabidhi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za SADC kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbuji kupitia Balozi wa Tanzania Nchini humo

“Agosti 17 mwaka huu mwenyekiti wa SADC anayemaliza muda wake Rais John Magufuli atakabidhi uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi kupitia balozi wa Msumbiji hapa nchini Monica Musa na makabidhiano haya yatafanyika jijini Dodoma.”

Rais Magufuli alikabidhiwa uenyekiti wa SADC Agosti mwaka jana kutoka kwa Rais wa Namibia Hage Geingob.

Mama Samia: Kiongozi mzuri anapita bila Rushwa
Makamu wa Rais atahadharisha rushwa Uchaguzi Mkuu