Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara yake inatekeleza programu ya uendelevu wa huduma ya Maji na usafi wa Mazingira Vijijini kwa kutumumia utaratibu wa malipo kwa matokeo (Program for Results – PforR), pamoja na nchi zaidi ya 40 dunia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia -WB.
Aweso ameyasema hayo wakati akiwasikisha maelezo ya utendaji wa Sekta ya Maji katika Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, yanayoratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi ya Uongozi na kudai kuwa awali ilipata dola 350 million na ndani ya miaka mitatu ilikuwa imepeleka maji kwa zaidi ya watu wapya 4.7 millioni Vijijini.
Amesema, upelekaji huo wa maji uliwezesha watu 6.6mil kuwa na vyoo bora Vijijini katika Mikoa 17 ikiwa ni matokeo makubwa kuliko nchi zote zinazotekeleza miradi kwa mpango wa matokeo chini ya Benki ya Dunia – WB ambayo imeiongezea fedha Tanzania kiasi cha Dola 300 milioni na sasa programu hiyo inatekelezwa kwenye mikoa 25 ikiwemo minane ambàyo awali haikuwemo.
Aidha, Aweso pia amewaomba Wakuu wa Mikoa kuipa ushirikiano thabiti kwa sekta ya Maji hususani katika kuendelea kazi nzuri kwenye programu hii ikiwa ni pamoja na kuwaomba kusimamia na kufuatilia Utekelezaji wa Miradi ya Maji ambapo tayari Shillingi Milioni 970 zimekwishapelekwa kwa kila Hamlamashauri zikiwa jumla ya 52 kwenye mikoa ambayo ilikua hainufaiki awali.
Kupitia programu hii ya lipa kwa matokeo (PforR) serikali kupitia Wizara ya Maji imetekeleza zaidi ya Miradi ya Maji 1,500 ambayo imekamilika na inatoa huduma.