Tanzania imeongoza kwa kuwa na Amani kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) inayotolewa na taasisi ya uchumi na amani (IEP)yenye makao yake makuu jijini Sydney nchini Australia.

Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na duniani ikiwa imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163, huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Jamhuri ya Czech ni nchi zilizoorodheshwa kuwa na amani zaidi duniani.

Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 , Kenya ya nne Afrika Mashariki na 28 katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Aidha, nchi zilizoshika nafasi za juu katika eneo la jangwa la sahara ni Mauritius, Botswana, Malawi, Ghana, Zambia na Sierre Leone.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi zilizo na kiwango cha chini cha amani ni Burundi, Chad, Cameroon, Mali, Nigeria, DR Congo, Somalia na Sudani Kusini.

Ripoti ya GPI inaonyesha kuwa dunia imekua na amani zaidi ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano ikiwa imepanda kwa asilimia 0.09.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa ongezeko la amani limetokana na kupungua kwa migogoro mikubwa duniani, hali iliyofanya kupungua kwa idadi ya vifo kutokana na migogoro ya ndani.

Mara ya mwisho ambapo dunia iliripotiwa kuwa na amani ni mwaka 2013 ambapo nchi 98 zilielezwa kufanya vizuri katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taasisi ya uchambuzi yenye makao makuu yake nchini Marekani Gallup World Poll (GWP), katika kipindi cha miaka kumi iliyopita imeshuhudia hali ya kuridhika kwa watu katika eneo la uhuru wa kuishi, kuheshimiwa na kuridhika na hali ya maisha.

Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zilirekodiwa kuwa na ongezeko la watu wenye msongo wa mawazo takriban asilimia 18 kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka 2018

Rais wa zamani wa Misri afariki baada ya kuanguka mahakamani
Mwanamazingaombwe apotelea mtoni akifanya onyesho