Tanzania ni nchi inayotumia ipasavyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kutokana na zaidi ya asilimia 50 ya kesi zilizoamuliwa kutoka nchini hapa.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Imani Aboud wakati wa kikao cha faragha kilichowakutanisha majaji wa nchi za Umoja wa Afrika, kutathimini utendaji kazi wa Mahakama.
Amesema, “kuna kesi tumezitolea maamuzi ya msingi maelekezo, ambazo ni 150 hadi sasa, lazima tuelewe kwamba maamuzi ya hii mahakama yanatoa miongozo kuwa uvunjaji wa haki za binadamu si wa nchi moja bali inatakiwa kufuatwa na nchi zote za Afrika.”
Aidha, Jaji Aboud amoengeza kuwa kesi ambazo zimetolewa maamuzi ya msingi na maelekezo madogo katika mahakama hiyo zipo 150, na zaidi ya asilimia 50 ya kesi hizo zimetoka Tanzania.