Kituo cha utafiti wa mbegu za asili (World Vegetable Center), kinatarajia kuanzisha benki ya mbegu asili ya mboga za majani (mnafu, mgagani na mlenda) nchini, kwa ajili ya kuzipeleka katika mikoa ambayo haina mboga hizo pamoja na nje ya nchi.

Mtafiti wa mbegu za mboga wa kituo hicho, Jeremiah Sigalla amesema kampuni ipo kwenye mikakati ya kuingia mikoa ambayo ina mnafu, mgagani na mlenda ili kuchukua mbegu na kuzitunza na baadae kuzisambaza mikoa mingine.

” Mboga za aina hiyo ni nzuri na zinapendwa na watu wengi, na zina faida nyingi ikiwemo kutoa vitamin kwa watu wanaotumia”. amesema Sigalla.

Sigalla ameongeza kuwa kituo hicho kimekuwa kikikusanya mbegu kutoka sehemu tofauti ili Tanzania ijitegemee kwa kila kitu katika masuala ya mbegu.

Sumaye: Wapuuzieni wanaowasema vibaya wagombea
Marekani yatuma ujumbe Tanzania kuhusu uchaguzi