Tanzania itaendelea kutoa mchango wake katika Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, ili kuwezesha utekelezaji mbalimbali wa miradi unaofanywa na mfuko huo, katika mageuzi katika sekta ya kilimo ni kipaumbele cha serikali ya Tanzania kwa kuwa inatambua umuhimu wake katika uchumi wa nchi.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko huo, Dkt. Geraldine Mukeshimana Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amesema, IFAD inatakiwa kuona umuhimu wa kuongeza eneo la mradi wa urejelezaji ardhi katika maeneo yanayokabiliwa na ukame Tanzania bara na Zanzibar na kuzingatia utoahi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji kulingana na uwekezaji halisi wa miradi, ili iweze kutekelezwa kwa wakati.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, Dkt. Geraldine Mukeshimana amesema Tanzania imekuwa ni mdau muhimu katika mfuko huo kwa kuwa mchangiaji mzuri na hivyo kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Ukatili si sehemu ya Maisha yako - Dawati la jinsia
Matumizi ya Ardhi ni endelevu, tuwajibike - Othman