Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia inahitajika kuwajengea watanzania uwezo na ujuzi ili wawekezaji wanapokuja kuwekeza nchini watanzania wafaidike moja kwa moja kwa kupata ajira na nafasi za juu.

Akizungumza na Dar24 Media Mwanauchumi Innocent Ndodyabike amesema kuwa mazingira ya uwekezaji anayoyatengeneza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ni tumaini kubwa la uchumi wa Nchi kukua kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa mazingira ya uwekezaji yanapowekwa vizuri yanawavutiwa wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

“Mfano Nchi ya China mji wa Xinjiang kilikuwa ni kijiji kidogo kinacholima mpunga lakini baada ya serikali kuligeuza eneo hilo kuwa la uwekezaji hii leo limekuwa ni jiji kubwa nchini China.” amesema Innocent.

Aidha, amezitaja faida za uwekezaji wa kutoka nje na ndani ni pamoja na uzalishaji wa bidhaa za ndani na za nje huongezeka na kutoa ajira nyingi kwa watanzania, faida nyingine bidhaa zinaweza zikaanza kuuzwa nje ya nchi na kupelekea kuongezeta kwa mapato.

Sambamba na hayo yote Mchumi Innocent amempongeza Rais Samia kwa juhudi zinazofanyika za uwekezaji na kutoa fursa kwa muwekezaji mkubwa Dangote kurudi na kuwekeza upy hii ni ishara nzuri katika uwekezaji.

CCM yalaani Catherine kuvamia msiba
Askari afa maji akimkimbiza mtuhumiwa