Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania inatarajia kupokea Marais 19 kutoka nchi za Jumuiya ya SADC huku wakiambatana na jumla ya wageni 1000, kwa ajili ya kushiriki mkutano wa jumuiya hiyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari, juu ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa SADC unaotarajia kufanyika Agosti 17, na 18 mwaka huu.

“Mwaka huu 2019 Tanzania itakuwa Mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika Agosti 17 na 18, na utatanguliwa na vikao vya awali kati ya Makatibu Wakuu na Mawaziri wa SADC, pia kutakuwa na maonyesho ya wiki ya viwanda kwa nchi za SADC kuanzia 22 hadi 26 Julai 2019, Wakuu wa nchi 19 watakuwepo hapa, jumla ya wageni watakuwa 1000,”amesema Prof. Kabudi

Aidha, mara ya mwisho Tanzania kuongoza Mkutano huo ilikuwa mwaka 2003, katika kipindi cha utawala wa Rais Mkapa ambapo mkutano huo mara nyingi umekuwa ukilenga kujadili masuala ya kiuchumi yanahusu nchi hizo.

Kaimu balozi wa Marekani avutiwa na fursa za uwekezaji Kagera
Wananchi vijijini watakiwa kushiriki shughuli za maendeleo