Prof (Dr.jur) Handley Mafwenga mwenye shahada tatu za uzamivu (PhD), na tatu nyingine za uzamili (masters), na miongoni mwa wasomi wenye shahada nyingi zaidi nchini hata duniani amesema anaichukulia Tanzania kuwa ni nchi ambayo itakuwa kuwa na nguvu kubwa kiuchumi kutokana na kasi ya ujenzi wa miundombinu.

Prof. Mafwenga ameyabainisha hayo wakati akihojiwa na kipindi cha exclusive cha Dar24 Media na akabainisha kuwa hali hiyo pia itachangiwa na kasi ya uendelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba uchumi wa Taifa la Tanzania upo kiushindani unaovisaidia Viwanda vya ndani.

“Sina shaka katika hili, uchumi wa Taifa utakuja kuwa tishio maana ina uchumi unaosaidia Viwanda vyetu vya ndani kujaribu kusaidia kukuza nguvu ya wawekezaji ili kuwa na ushindani katika soko la Kimataifa na ni uchumi ambao unalinda thamani ya shilingi ya Kitanzania,” amefafanua Prof. Mafwenga.

Prof (Dr.jur) Handley Mafwenga.

Ameongeza kuwa, wachumi wa Taifa la Tanzani awanatakiwa kufanya tathmini ya hali ya uchumi nchini kwa kulinganisha kipindi cha nyuma na hasa kwa kuzingatia kuwa nchi imepitia vipindi vingi tangu kupata uhuru mwaka 1961 ingawa hali ilivyo haiendani na kile kitachotarajiwa kutokana na makusanyo ya mbalimbali.

Tangu alipojiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuhitimu diploma ya juu ya kodi (advanced diploma) mwaka 1987, Prof. Mwafwenga hajawahi kuacha kusoma kiasi cha watu wake wa karibu kumshauri apumzike.

Simba SC kumpotezea Muethiopia
Adebayor aipeleka Simba SC Morocco