Ushindi wa Simba SC dhidi ya FC Platinum ya Zimbambwe umeiwezesha Tanzania kupanda nafasi moja juu, kutoka ya 13 hadi ya 12, kwenye viwango vya Ligi Bora barani Afrika.

Simba SC ilibugiza FC Platinum ya Zimbabwe mabao manne kwa sifuri, katika mchezo wa mkondo wa pili wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika jana Jumatano (Januari 06), Uwanja Taifa Dar es salaam.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Desemba 23-2020 mjini Harare Zimbabwe, Simba SC walifungwa bao moja kwa sifuri, hivyo matokeo ya jumla yanaifanya klabu hiyo ya Tanzania kusonga mbele kwa jumla ya mabao manne kwa moja.

Ligi 12 bora za Afrika ndizo hupewa nafasi 4 za uwakilishi kwenye michuano ya Afrika (Mbili Ligi ya Mabingwa na Mbili Kombe la Shirikisho).

Hii ina maana kwamba msimu ujao wa mashindano ya Afrika, 2021/22, Tanzania itatoa timu 4 kama ilivyokuwa msimu wa 2019/20.

Hata hivyo Tanzania itapata nafasi hiyo endapo Al Alhly Benghazi ya Libya ambayo imetolewa Ligi ya Mabingwa kuangukia Shirikisho, itafika mbali zaidi na timu zetu zikaishia hapo zilipo.

Uganda yapiga marufuku simu katika uchaguzi
Maalim Seif akemea ubaguzi wa rangi Zanzibar

Comments

comments