Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha hapa nchini ambao utapatikana kwa gharama nafuu.
Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Pwani leo 18 Novemba kwenye uzinduzi wa njia ya mchepuko kupitishia maji kwenye mradi wa ufuaji umeme wa Julius Nyerere Majaliwa amesema kuwa serikali itaipa kipaumbele sekta ya nishati ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa umeme inaimarika kama njia mojawapo ya kusogeza huduma za kujamii na maendeleo kuwafikia wananchi.
Amesisitiza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa bei nafuu utachochea ukuaji wa sekta ya viwanda kwa kushusha gharama za uendeshaji jambo litakalosaidi kukabiliana na mfumuko wa bei.