Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, vijana na Watu wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amewasilisha salamu za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan, na kueleza juhudi anazozifanywa katika kupambana na madhara ya UVIKO -19 kwenye soko la ajira.

Ndalichako ametoa salam hizo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), na kulipongeza kwa namna lilivyojipanga kusaidia nchi zinazoendelea katika bajeti zijazo ikiwepo kuonesha utayari wa Tanzania katika ushirikian ili kutatua changamoto za soko na fursa za ajira kwa vijana, kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii, kusimamia viwango vya kazi na kuimarisha uhuru wa majadiliano kati ya waajiri na wafanyakazi.

Aidha amezitaja juhudi zilizofanywa na Serikali ya Tanzania za kutatua changamoto ya soko la ajira kuwa ni uanzishwaji na utekelezwaji wa programu ya taifa ya kukuza ujuzi, ambayo imewezesha vijana walio katika mazingira magumu wakiwemo walemavu kupata fursa ya mafunzo ya ujuzi wa kufanya kazi, kusimamia uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi na kaguzi sehemu za kazi.

Jitihada nyingine ni pamoja na kuwezesha Bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta ya Umma na binafsi na maboresho katika sekta ya Hifadhi ya jamii ikiwemo kujali maslahi ya wafanyakazi.

Hofu yatanda kukamatwa bunduki 200, risasi 3,000
Wanahabari wapaza sauti maboresho ya sheria