Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki ameongoza ujumbe wa Tanzania uliofanya ziara ya kikazi Jimbo la Oromia nchini Ethiopia, kujifunza kuhusu kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao ya chakula na biashara.

Akizungumza katika ziara hiyo, inayoendelea nchini Ethiopia, Waziri Kairuki amesema Tanzania itaongezea uzoefu kutoka Ethiopia kwa pale ilipokuwa imeanza kwa kujikita kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya ngano, alizeti, mpunga, soya, mahindi, parachichi, zabibu na viazi mviringo.

Mazao hayo yameanishwa na kuchaguliwa kwa kuzingatia mchango wake katika maeneo makuu manne ya vipaumbele nchini Tanzania, ikiwemo usalama wa chakula, kutengeneza ajira, kuongeza fedha za kigeni, na kuwa mbadala wa mazao yanayoagizwa kwa wingi kutoka nje.

Jimbo la Oromia limefanya vizuri katika utekelezaji wa mradi wa kuwezesha wakulima kupitia mnyororo wa thamani wa mazao ya ngano, parachichi na kahawa ambapo katika ziara hiyo, Kairuki ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwekezaji Tausi Mbaga Kida pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Iringa na Mbeya.

Waandishi waaswa uhuru wa kujieleza, ajenda haki za Binadamu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 4, 2023