Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof . Emmanuel M.L. Mbennah amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Prithvirajsing ROOPUN, G.C.S.K, Rais wa Jamhuri ya Mauritius, Ikulu mjini Port- Luis, Mauritius.

Balozi Profesa Mbennah amewasilisha salam kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia_Suluhu_Hassan kwenda kwa Prithvirajsing ROOPUN , G.C.S.K, Rais wa Jamhuri ya Mauritius.

Aidha , Balozi. Profesa Mbennah amepata wasaa wa kufanya mazungumzo ya faragha na Rais kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Mauritius hususan kuhusu utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi, ukamilishaji wa Mikataba mbalimbali ukiwemo Mkataba wa Jumla.

Obama atoa wito kwa vijana kupambana na mabadiliko ya tabia nchi
Sekta ya Madini yazidi kuneemeka kiuwekezaji