Tanzania inajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika, unaotarajia kufanyika Jijini Arusha Oktoba 23 hadi 27, 2023.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo, kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu.

Amesema, mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuzitaja Nchi  wanachama wa jukwaa hilo kuwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe, Eswatini, Msumbiji, Seychelles, Botswana.

Nyingine ni Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini ambapo mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu isemayo “Jukumu la Mahakama za Nchi Wanachama katika Utatuzi wa Migogoro chini ya Utangamano wa eneo Huru la Biashara la Afrika: Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa kwa Ufanisi katika Utoaji Haki.”

Mgomo kupinga gharama za maisha waanza rasmi
Mikakati kutangaza vivutio vya Utalii kuendelezwa