Serikali za Tanzania na Finland, zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta zenye maslahi mapana ya kiuchumi kwa wananchi wa nchi hizi mbili ikiwemo biashara, utalii na uwekezaji.
Ahadi hiyo, imetolewa katika mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Uchumi wa Finland, Mika walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 31 Januari 2023.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Finland kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 19 wa Nchiza Nordic na Afrika uliofanyika mwezi Juni 2022. Pia ameeleza kuwa Tanzania
itaendelea kushiriki kwenye majukwaa mbalimbali ili kuwasilisha mchango wake katika masuala ya kikanda na kimataifa.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, utalii, teknolojia ya habari na mawasiliano, usafirishaji, afya, kilimo, madini, nishati, elimu, mazingira na tafiti ili kupitia sekta hizo wananchi hususan wa Tanzania wanufaike kiuchumi na kijamii.