Tanzania imepanda nafasi nane kwenye mwenendo wa ubunifu dunia (Global Innovation Index ) kutoka nafasi ya 97 mpaka nafasi ya 88 mwaka 2020 kidunia, na nafasi ya nne katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya TCU yaliyofungwa Septemba 5, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu, amesema ripoti hiyo inaifanya Tanzania kupiga hatua katika swala nzima la ubunifu hapa nchini.

Amesema, Tanzania kupiga hatua kwenye suala zima la ubunifu inamaanisha ndoto za uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda unaendelea kuonekana

“Kama ubunifu unapanda kwa kasi na dunia inatambua hilo ina maana uchumi wa viwanda unadhihirika wazi,” amesema Nungu.

Aidha, Nungu amewaasa wadau wa elimu ya juu kufundisha teknolojia kwa vitendo badala ya nadharia na kubuni kwa tija.

Kagera kuongoza uzalishaji wa kahawa
Hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM- Bashiru