Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Julai 7, 2022 ameshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Africa, zinazonufaika na dirisha la International Development Association (IDA), katika Ukumbi wa Hotel ya King Fahd Palace jijini Dakar nchini Senegal.

Zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio tofauti wakati wa Mkutano huo, na wakati Rais Samia alipowasili nchini humo Julai 6, 2022 na kukutana na mwenyeji wake Rais wa Senegal, Macky Sall.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Wakuu wa nchi mbalimbali wa Afrika katika Mkutano wa faragha wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa (IDA 20 Summit for Afrika) uliofanyika Dakar nchini Senegal Julai 7, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika mara baada ya Mkutano wa Wakuu hao wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa (IDA 20 Summit for Afrika) Dakar nchini Senegal Julai 7, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall Julai 6, 2022 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo la Kimataifa (IDA 20 Summit for Afrika nchini Senegal.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa (IDA 20 Summit for Afrika) uliofanyika kwenye ukumbi wa King Fahd Palace Dakar nchini Senegal Julai 7, 2022.

Wachimba madini watakiwa kusafisha Dhahabu nchini
Watumishi wa umma kupimwa kwa utendaji