Klabu ya Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ imesema itasajili wachezaji sita tu kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu huku ikipanga kuingia kambini Julai 15.

Akizungumza jana, Msemaji wa klabu hiyo, Jackson Mwafulango, amesema kwa mujibu wa ripoti ya mwalimu Mohamed Abdallah ‘Bares’, wanahitajika wachezaji sita, huku tayari wakiwa wameshawapa mkono wa kwa heri wachezaji wanne mpaka sasa.

“Tutasajili wachezaji sita, sitotaja majina hapa nitazitaja nafasi zao, beki wa kati mmoja, kiungo mshambuliaji, washambuliaji wawili namba tisa na namba kumi, winga mmoja na kipa mmoja, lakini hii ya golikipa tunasubiri ripoti ya daktari juu ya kipa wetu Musa Mbissa ambaye aliumia kwenye mechi za mwisho za msimu uliomalizika, amesema Mwafulango.

Aidha, amesema kama daktari wa timu hiyo atasema golikipa wao huyo yuko fiti hawatasajili golikipa mwingine.

Pia alibainisha safari hii wanataka kufanya ‘pre season’ ya nguvu ili kuleta ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu msimu ujao ambayo anaamini kuwa itaku- wa ngumu.

“Safari hii kuelekea msimu ujao tunataka kufanya ‘pre season’ ya nguvu, viongozi wa juu wamesema maandalizi yaanze mapema na tuchague sehemu ya kuweka kambi yetu kwa ajili ya maandalizi hayo,” amesema Mwafulango.

Amesema Miji ambayo imetajwa kuwa mmoja wapo watakwenda kuweka kambini, Musoma mkoani Mara, Mwanza, Zanzibar au Dar es Salaam.

“Kati ya miji hiyo niliyoitaja, mmoja wapo ndiyo tutaweka kambi, tutaanza Julai 15 na itakuwa ni ya wiki mbili au tatu kabla ya kuanza ligi, kwa sasa kocha Bares yupo mapumzikoni nyumbani kwao Zanzibar, huku Mbeya mazoezi yameshaanza chini ya Kocha Msaidizi, Shaabn Mtupa,” amesema.

Tayari Prisons imeshawapa ‘thank you’ wachezaji Oscar Paul, Ismail Mgunda, Ramadhani Ntobi na Michael Masinda, huku Shaaban Kisiga akipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Magereza Dar.

Rais Paris Saint-Germain amtega Kylian Mbappé
Declan Rice kutumika tofauti Arsenal