Klabu ya Tanzania Prisons imetangaza kuwaacha wachezaji 16 kwenye usajili wa msimu ujao 2021/22, unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba.
Prisons imethibitisha kuachana na wachezaji hao, baada ya kukamilisha mchakato wa kujiridhisha nani anayepaswa kuendelea kukipiga klabuni hapo.
Baadhi ya wachezaji walioachwa wamemaliza mikataba yao na wengine wameachwa kutokana na kutokuwa sehemu ya mipango ya benchi la ufundi ya msimu ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania wachezaji walioachwa ni Jeremiah Kisubi (Kipa), Andrew ntala (Kipa), Prosper Kaini (Kipa), Steven Mwaijala. (Beki wa kushoto), Nicodem Mwaipaja (Beki wa kati), Seleman Mangoma (Kiungo mshambuliaji), Hamidu Mohamed (Kiungo), Francis Joel (Kiungo) na Salumu Bosco (Mshambuliaji).
Wengine ni Kassim Mdoe (Kiungo mshambuliaji), Stamili Mbonde (Mshambuliaji), Gasper Mwaipasi (Kiungo mshambuliaji), Ramadhan Ibata (Mshambuliaji), Kennedy kipepe. (Beki), Shaban William. (Kiungo) na John Sungura (Beki).
Wakati huo huo Uongozi wa Tanzania Prisons unaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji watatu, ili kuwaongezea mikataba ya kuendelea kufanya kazi klabuni hapo.
Wachezaji hao ni Adili Buha, Shadrack Thomas na Mohamed Mkopi.