Uongozi wa Tanzania Prisons umewatoa hofu Mashabiki wake kwa kuwataka kuendelea kukiamini kikosi chao, licha ya kusuasua kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Maafande hao wa Jeshi la Magereza wamekua na matokeo mabaya msimu huu, huku wakiburuza mkia wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hali ambayo imezua taharuki kwa mashabiki ambao wanahisi huenda timu yao ikashuka daraja msimu huu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Tanzania Prisons Jackson Mwafulango amesema Uongozi unaendelea kupambana ili kurejesha makali kwenye kikosi chao, na wanaamini zoezi hilo litaleta matokeo chanya.

Amesema kinachowatokea kwa sasa ni upepo mbaya wa kupata matokeo yasiyoridhisha, hivyo wanaendelea kutafuta dawa itakayowasiadia ili kurejea katika kiwango chao na kushinda michezo 14 iliyosalia.

“Uongozi wa Tanzania Prisons unaendelea kupambana usiku na mchana ili kuondoakana na hali hii, hairidhishi kwa kweli, tunaamini matokeo yanayotuandama kwa sasa ni sehemu ya upepo mbaya uliotukumba.”

“Tumebakisha michezo 14, tunaamini katika michezo hii timu itakua na mtazamo tofauti na itaanza kupata matokeo ambayo yatatuondoa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu, na kurejea katika nafasi zetu tuliozoeleka.” Amesema Mwafulango.

Jana Jumanne (Machi 15), Tanzania Prisons ilipoteza mchezo 11 msimu huu, kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United Mara iliyokua nyumbani katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Tanzania kusikika mkutano wa 66 wa hali ya wanawake duniani
Lusajo: Sina mpango wa kushindana, natamani kufunga zaidi