Waziri wa Maliasili na Utalii Khamisi Kigwangala leo Jumanne (Agosti 11-2020), amezindua rasmi Muhuri wa usalama kutoka Baraza la usafiri na Utalii dunia *WTTC* uliopokelewa nchini Julai 22 mwaka huu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Muhuri huo jijini Dar es salaam, Waziri Kigwangala ameushukuru uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa umahiri ulionekana kwa kuthibiti ugojnwa wa Covid 19, na kupelekea Tanzania kufungua mipaka huku tukichukua hatua madhubuti katika kujinga na ndio sababu kubwa inatufanya leo kuwa hapa na kutumia muhuri wa usalama.

Aidha Kingwangala amempongeza katibu mkuu mpya wa wizara ya maliasili na utalii Aloyce Nziku kwa juhudi walizozifanya katika kipndi chote cha Covid 19, kwa kutokusita kushirikiana na balozi za Tanzania kuifikia dunia na kutangaza utalii wa Nchi.

“Kama mnakumbuka mwezi juni mwaka huu ninilipozindua muongozo wa namna bora wa kuendesha shughuli za utalii wakati wakati wa janaga la covid 19 nilizungumza umuhimu wa kuitaarifu tanzania ni salamatunafuraha leo kuona juhudi hizo zimezaa matunda.” amesema Waziri Kingwangala.

Amesema Tanzania imeorodheshwa miongoni mwa vivutio salama duniani na kuthibitishwa kutumia muhuri wa usalama uliotolewa na Baraza hilo sambamba na utambulisho wa nchi Unforgettable Tanzania Destination logo.

Maandamano yamng'oa Waziri Mkuu Lebanon
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 11, 2020