Mabingwa wa Michuano ya CECAFA Challenge 2021 Timu ya Taifa ya Tanzania U23 wamewasili nchini mapema leo Jumapili (Agosti Mosi) wakitokea Ethiopia.
Tanzania U23 walitwaa Kombe hilo juzi Ijumaa (Julai 30) baada ya kuifunga Burundi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 huko Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania *TFF* Wilfred Kidao ameongoza timu ya mapokezi kwa Mabingwa hao Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokea kombe la Ubingwa.