Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg.

Mazungumzo ya Dkt. Ndumbaro na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.

Balozi Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako kinachopatikana katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

“Kupitia uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za ajira kwa mataifa haya mawaili,” Amesema Balozi Acker.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha uhusiano wake na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg. Viongozi hao walizungumza kuhusu namna ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinapiga hatua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao jijini Dar es Salaam

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na Sweeden katika Sekta mbalimbali hasa katika wakati huu ambao Tanzania inapiga hatua kuelekea uchumi wa viwanda.

CORONA: TFF waitana kwa dharura
HOFU YA CORONA: Wafungwa 1,350 watoroka, wateka askari (Video)