Tanzania imeweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuandaa Mkutano wa Kimataifa wa Manunuzi ya Umma (IPPC) ulioanza jana jijini Arusha.
Mkutano huo wa 18 wa IPPC, uliofunguliwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango umehudhuriwa na wadau wa manunuzi ya umma pamoja na wataalam wa uchumi takribani 500 kutoka nchi 55 duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kufungua mkutano huo mkubwa, Dkt Mpango alisema kuwa ni heshima kwa Tanzania kupewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa duniani na kwamba hiyo inatokana na kazi nzuri ya kusimamia na kudhibiti manunuzi ya umma inayofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
“Bado kuna changamoto lakini tumepiga hatua ikiwa ni pamoja kuimarisha udhibiti na usimamizi wa manunuzi ya umma. PPRA ambaye ndiye msimamizi wa eneo hili anakagua taasisi mbalimbali kila mwaka na pale ambaPo pana viashiria vya matumizi mabaya basi hao utaratibu wetu ni uleule, tunawapeleka kwenye vyombo vya kiuchunguzi ili wakaimbe muziki wao wanaostahili kwa kutumia vibaya fedha za umma,” alisema Dkt Mpango.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Dkt Samuel Werema, ambaye ni kaimu mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), alisema kuwa katika mkutano huo wataalm wa masula ya manunuzi kutoka nchi 50 watajadili changamoto zinazoikabili sekta na utatuzi wake.
Alisema kuwa ni heshima kubwa kwa Tanzania kuchaguliwa kati ya nchi 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Afrika, kuwa wa kwanza kuandaaa mkutano huo.
JPM atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha ‘King Majuto’
Mkutano huo wa siku tatu, ulioanza jana utahitimishwa Agosti 10. Umeandaliwa kwa ushirikiano wa taasisi wadau wa manunuzi ya umma ambao ni PPRA, PSPTB, PPAA, GPSA na IAA. Mkutano wa IPPC uliopita ulifanyika nchini Indonesia mwaka 2016.