Shirikisho la soka duniani FIFA leo limetoa orodha ya Viwango Vya Ubora wa Soka huku Tanzania, ikishika nafasi ya mwisho katika ukanda wa Afrika mashariki.
Kwa mujibu wa orodha ya viwango vya ubora vya FIFA, Afrika mashariki inaongozwa na Uganda inayoshika nafasi ya 78 (Duniani), ikifuatiwa na Kenya inayoshika nafasi ya 105 (Duniani), Rwanda ni ya tatu bada ya kushika nafasi ya 112 (Duniani) na Tanzania ikiwa mkiani katika nafasi ya 146.
Bara la Afrika linaongozwa na nchi ya Tunisia inayoshika nafasi ya 23 duniani, ikifuatiwa na Senegal (27), Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (39), Morocco (42), Misri (44), Cameroon (51), Nigeria (52), Ghana (54), Burkina Faso (56), Algeria (60) na visiwa vya Cape Verde (61).
Kwa upande wa dunia.
1: Germany
2: Brazil
3: Portugal
4: Argentina
5: Belgium
6 :Poland
7: Spain
8: Switzerland
9: France
10: Chile